Psalms 37

Mwisho Wa Mwovu Na Urithi Wa Mwenye Haki

(Zaburi Ya Daudi)


1
Zaburi hii imetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
bUsisumbuke kwa ajili ya watendao maovu,
wala usiwaonee wivu watendao mabaya,

2 ckwa maana kama majani watanyauka mara,
kama mimea ya kijani watakufa mara.


3 dMtumaini Bwana na utende yaliyo mema;
Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.

4 eJifurahishe katika Bwana
naye atakupa haja za moyo wako.


5 fMkabidhi Bwana njia yako,
mtumaini yeye, naye atatenda hili:

6 gYeye atafanya haki yako ing’ae kama mapambazuko,
na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri.


7 hTulia mbele za Bwana
na umngojee kwa uvumilivu;
usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao,
wanapotekeleza mipango yao miovu.


8 iEpuka hasira na uache ghadhabu,
usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu.

9 jKwa maana waovu watakatiliwa mbali,
bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.


10 kBado kitambo kidogo, nao waovu hawataonekana,
ingawa utawatafuta, hawataonekana.

11 lBali wanyenyekevu watairithi nchi
na wafurahie amani tele.


12 mWaovu hula njama dhidi ya wenye haki
na kuwasagia meno,

13 nbali Bwana huwacheka waovu,
kwa sababu anajua siku yao inakuja.


14 oWaovu huchomoa upanga
na kupinda upinde,
ili wawaangushe maskini na wahitaji,
kuwachinja wale ambao njia zao ni nyofu.

15 pLakini panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe,
na pinde zao zitavunjwa.


16 qBora kidogo walicho nacho wenye haki
kuliko wingi wa mali wa waovu wengi;

17 rkwa maana nguvu za waovu zitavunjwa,
lakini Bwana humtegemeza mwenye haki.


18 s Bwana anazifahamu siku za wanyofu,
na urithi wao utadumu milele.

19 tSiku za maafa hawatanyauka,
siku za njaa watafurahia wingi wa vitu.


20 uLakini waovu wataangamia:
Adui za Bwana watakuwa
kama uzuri wa mashamba,
watatoweka,
watatoweka kama moshi.


21 vWaovu hukopa na hawalipi,
bali wenye haki hutoa kwa ukarimu.

22 wWale wanaobarikiwa na Bwana watairithi nchi,
bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali.


23 xKama Bwana akipendezwa na njia ya mtu,
yeye huimarisha hatua zake,

24 yajapojikwaa, hataanguka,
kwa maana Bwana
humtegemeza kwa mkono wake.


25 zNilikuwa kijana na sasa ni mzee,
lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa
au watoto wao wakiombaomba chakula.

26 aaWakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti.
Watoto wao watabarikiwa.


27 abAcha ubaya na utende wema,
nawe utaishi katika nchi milele.

28 acKwa kuwa Bwana huwapenda wenye haki
naye hatawaacha waaminifu wake.

Watalindwa milele,
lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali.

29 adWenye haki watairithi nchi,
na kuishi humo milele.


30 aeKinywa cha mwenye haki hutamka hekima,
nao ulimi wake huzungumza lililo haki.

31 afSheria ya Mungu wake imo moyoni mwake;
nyayo zake hazitelezi.


32 agWatu waovu huvizia wenye haki,
wakitafuta kuwaua;

33 ahlakini Bwana hatawaacha mikononi mwao
wala hatawaacha wahukumiwe
kuwa wakosa wanaposhtakiwa.


34 aiMngojee Bwana,
na uishike njia yake.
Naye atakutukuza uirithi nchi,
waovu watakapokatiliwa mbali,
utaliona hilo.


35 ajNimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi
kama mwerezi wa Lebanoni,

36 aklakini alitoweka mara na hakuonekana,
ingawa nilimtafuta, hakupatikana.


37 alWatafakari watu wasio na hatia,
wachunguze watu wakamilifu,
kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.

38 amLakini watenda dhambi wote wataangamizwa,
mafanikio yao yatakatiliwa mbali.


39 anWokovu wa wenye haki hutoka kwa Bwana,
yeye ni ngome yao wakati wa shida.

40 ao Bwana huwasaidia na kuwaokoa,
huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi,
kwa maana wanamkimbilia.
Copyright information for SwhKC